أَقِمِ الصَّلاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلى غَسَقِ اللَّيْلِ وَ قُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كانَ مَشْهُوداً
(Simamisha
Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri.
Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima.) QURAN 17/87
MAFUNZO YA SWALA SAHIHI
Kwanza kabisa,lazima mwenye kuswali ahakikishe ametoa Adhana kisha Iqama(yaani:Kukimu kwa ajili ya kusimamisha swala).
Baada ya ADHANA na IQAMA basi hapo inafuatia TAKBIRATUL-IHRAM (الله أکبر).
Swala inaanza kwa kutamka Takbir hii, ukisha itamka basi hapo tayari swala imeanza na inaisha kwa kutoa salam.
Baada ya utangulizi huu mfupi, sasa ni wakati wa kuyatizama yale mambo ambayo ni wajibu katika swala.
MAMBO YA WAJIBU KATIKA SWALA
Mamabo
yawajibu katika swala ni kumi na moja (11).Lazima mwenye kuswali
ahakikishe mambo hayo kumi na moja ameyatenda kama inavyotakiwa.Katika
mambo haya kumi na moja (11) ya wajibu kuna matano (5) ni RUKNI
(Yaani:Ni nguzo za Swala) na mengine sita(6) yaliyobaki si RUKNI katika
swala.Na inaposemwa “RUKNI ZA SWALA”,humaanishwa NGUZO ZA SWALA,kwa
maana kwamba:Swala imesimama katika nguzo hizo tano,ikitokea nguzo moja
ikaharibika au isitendeke kama inavyotakiwa au ikasahaulika katika swala
basi swala itakuwa si sahihi,mwenye kuswali atatakiwa kurudia swala
yake,ama yale mambo sita(6) ambayo sio nguzo za swala,ikitokea moja wapo
kati ya hayo (sita) ikasahaulika ktk swala au kutendeka isivyotakiwa
basi swala haitaharibika au tuseme:Haitakuwa batili,bali itakuwa ni
swala sahihi,maana kukosea au kusahau katika hayo mambo sita ambayo si
nguzo ktk swala hakuharibu swala wala kuibatilisha,ispokuwa makosa hayo
au kusahau huko kukitokea ktk moja wapo ya nguzo za swala ambazo
tutazitaja hivi punde.
MAMBO YA WAJIBU KTK SWALA NA AMBAYO NI RUKNI ZA SWALA/ NGUZO ZA SWALA
Nguzo za swala ni tano:
1- NIA
Nia
si lazima utamke kwa maneno kwamba,nina swali swala ya dhuhri yenye
rakaa nne,kurbatan ila llah,si lazima uimbe nia namna hiyo bali nia
inatosha kile ulichokiazimia moyoni mwako,maana ile kuchukua maji,ukatia
udhu,tayari ushajenga nia ktk moyo wako na ktk akili yako kwamba sasa
naelekea kwenye swala fulani.Nia maana yake ile azma yako kunako
unachotaka kukitenda,si sharti uanze kuitaja kwa maneno.Mfano;Msafiri
anaetaka kuelekea sehemu fulani,huwa anatia nia kuwa kesho au sasa hivi
ninasafiri kuelekea sehemu fulani,nia hiyo huwa ipo moyoni,na ile kutoka
kuelekea kituo cha basi hutosha kabisa kudhihirisha nia yake ya safari
yake.
Hivyo
nia hutimia pasina kutamkwa na ile kutakwa sio sharti ktk Nia,bali
unaweza kuitamnka tu kwa ulimi na isitimie,maana kutimia kwa nia ni pale
inapohudhuria moyoni kiasi kwamba akili ya mwenye kuswali inakuwa
haiwazi kitu kingine tofauti na swala na kwamba sasa yupo mbele ya
Mwenyeezi Muingu (s.w).Hiyo ndiyo nia ambayo unatakiwa kuileta mwanzo wa
swala na iendelee kuwepo hadi mwisho wa swala.Hivyo nia sio mwanzo wa
swala tu bali iwepo hadi mwisho kabisa wa swala yako.
2- QIYA’M (Kusimama wima).
3- TAKBIRATUL-IHRAM(Takbir ya kuhirimia swala na ambayo inaashiria mwanzo wa swala kwamba sasa swala imeanza).
4- RUKUU (Kurukuu).
5 - SUJUD (Kusujudu).
MAMBO YA WAJIBU KTK SWALA NA AMBAYO SIO RUKNI ZA SWALA/ SIO NGUZO ZA SWALA
6- Qira’a :(Kusoma Suratul Fatiha,yaani:Al-Hamdu,kisha Sura yoyote).
Sura
unayoisoma lazima uisome kuanzia mwanzo hadi mwisho,hairuhusiwi kusoma
sura nusu,rakaa ya kwanza kisha kusoma nusu iliyobaki katika rakaa ya
pili.Bali inatakiwa isomwe sura kamili mwanzo hadi mwisho.Mfano
huruhusiwi kusoma KULI HUWALLAH AHAD NUSU YAKE NA KUMALIZIA NUSU
ILIYOBAKI KATIKA RAKAA YA PILI,NA HIVYO HIVYO KTK SURA YOYOTE ILE
UTAKAYOISOMA KTK SWALA.
Hapa
lazma tuweke wazi:Ukichunguza swala za walio wengi ktk madh-hebu ya
Ahlus-sunna,utakuta baada ya kusoma Al-hamdu,basi mtu anasoma sura
yoyote ndefu kama Suratul-Baqarah kama Aya kumi kisha anarukuu,kisha
anarudi rakaa ya pili anasoma Aya zingine kama ishirini au kumi na tano
au zozote atakazoweza kutoka sura nyingine kama vile Suratun-Nisaa kisha
anaurukuu!.Lakini kwa mujibu wa mafunzo sahihi tunayofundishwa
au iliyofundishwa na Maimam wetu watukufu (a.s) kutoka Nyumba ya Mtume
(s.a.w.w) ambao hakuna shaka yoyote (wala chembe ya shaka kwamba)
wanaijua vizuri zaidi swala ya Mtume (s.a.w.w),swala sahihi lazima ktk
QIRAA isomwe sura kamili ana sio nusu sura au robo yake au nusu robo.Na
hivyo ni bora mwenye kuswali au kuswali kama Imam asome sura fupi ktk
swala ambazo atakuwa na uwezo wa kuzisoma mwanzo hadi mwisho na sio
kusoma sura ndeeefu wakati anajua anawaongoza watu ambao wanatofautiana
hali zao za kiafya.Hivyo zisomwe sura kamili na sio nusu sura,ktk qur’an
sura fupi zimo nyingi sana unazoweza kuzisoma kwa ukamilifu kama vile
Suratun-naziat,surat
Abas,surat-tak-wiyr,suratul-infi-twaar,suratul-mutwaffifiin,suratul-inshiqaaq,suratul-buruuji,Suratu-twaariq,suratul-a’ala,suratul
ghashiya,suratul-fajri,suratul-balad,suratul-lail,suratul-qadr,suratul-bayyina,suratul-kaafirun,suratun-nasri,suratul-ikhlaaswi,suratul-falaq,suratun-naasi,na
zingine nyingi tu.
7-Dhikr
8-Tashahhud
9-Salam
10-Tartib:
(Kwa maana kwamba:Swala lazimwa iswaliwe kwa kufuata utaratibu
huu,kuanzia Takbiratul-Ihram,kisha hatua Qira’a,kisha Rukuu,kisha
sujud,kisha ukae ktk rakaa ya pili baada ya sajda usome
TASHAHUD,ukimaliza ndio usimame kwa kwa ajili ya rakaa ya tatu,kisha
ukae ktk rakaa ya mwisho usome TASHAHUD,na baada ya Tashahud
umalizie kwa Salam,swala inatakiwa iwe ktk utaratibu huo au tuseme
ifuate utaratibu huo,sio unaanza na Takbiratul-Ihram,kisha unaingia
sajda,unaacha qira’a na rukuu,namna mwenye kuswali atakuwa hajafuata
utaratibu,na atahesabika anaswali anavyotaka na sio inavyotakiwa).
11-Muwalaat:
Yaani: Lazima mwenye kuswali ahakikishe anaswali swala yake kwa
kufuatanisha vitendo pasina kuacha gape au nafasi bain aya kitendo na
kitendo.Mfano:Baada ya Takbiratul-ihram,unaingia moja kwa moja kwenye
Qira’a na baada ya Qira’a Al-hamdu na sura na baada ya hapo unaingia
moja kwa moja kwenye Rukuu,namna hiyo.Hivyo haitakiwi kutoa
Takbiratul-Ihram kisha kukaa kama dakika tano kama haupo kwenye swala
kisha ndio usome Al-hamdu na sura kisha baada ya kurukuu unakaa kama
dakika zako kumi ndio unaamua kurukuu,namna hiyo utakuwa hujafatanisha
vitendo ktk swala,bali kwa kuachanisha vitendo namna hiyo maana ya swala
inapotea kabisa na utatoka nje ya swala na kubatilisha swala yako.Na
hataka kusoma sura ndefu kama vle suratul-baqara ukiig’ang’ania mpaka
uimalize hatua hiyo inaondoa kabisa ufuatanishaji wa vitendo ktk
swala,na ndio ikawa ni bora kusoma sura fupi ktk swala kwa kuzikamilisha
na sio nusu yake.
DHIKRI KTK RUKUU
Ukiwa
ktk Rukuu,umenyoosha mgongo wako,na macho yako yametizama sehemu ya
kusudu, unatakiwa kusoma dhikri hii: “SUBHANA RABIYAL-ADHIMI WABIHAMDIH” (سبحان ربِّيَ العاظيمِ وَبحَمدِهِ) mara moja,au kama hujasoma dhikri hiyo basi usome:SUBHANALLAHI (سُبحانَ اللهِ) kwa kurudia mara tatu na sio chini ya hapo au zaidi ya hapo.
DHIKRI KTK SAJDA:
Ukiwa katika Sajda,katika hali ya utulivu,huku viungo vyako saba vya sajda vikiwa vimegusa ardhini,unatakiwa kusoma dhikri hii: SUBHANA RABIYAL-A’ALA WABIHAMDIH” (سبحان ربِّيَ الأعلی وَبحَمدِهِ) mara moja,au au kama hujasoma dhikri hiyo basi usome:SUBHANALLAHI (سُبحانَ اللهِ) kwa kurudia mara tatu na sio chini ya hapo au zaidi ya hapo.
DHIKRI KATIKA TASHAH-HUD
Katika
swala,ndani ya Rakaa ya pili na mwisho wa swala,inatakiwa baada ya
Sajda ya Rakaa ya pili mwenye kuswali akae,na akiwa ktk hali ya utulivu
wa mwili,asome Tashah-hud kama ifuatavyo:
ASH-HADU
ANLA-ILAHA ILLAH LLAH WAHDAHU LA SHARIKA LAHU,WA ASH-HADU ANNA
MUHAMMADAN ABDUHU WARASULULLLAH,ALLAHUMMA SWALLI ALA MUHAMMADIN WA A’LI
MUHAMMAD.
أشهدُ أن لا إله إلا اللهُ وَحدَهُ لا شَرِيک لهُ وأشهدُ أنَّ محمَّداً عبدُهُ وَرَسُولُهُ اللهُمَّ صلِّ علی محمَّدٍ وَ آل محمَّدٍ.
Huo
ndio mwisho wa Tashah-hud ktk rakaa ya pili baada ya Sajda,hapo
utatakiwa kusimama kwa ajili ya kuleta rakaa ya tatu,na kama swala yako
ni ya rakaa mbili basi baada ya tashah-hud hiyo utatakiwa kufuatisha
Salam (AMBAYO NDIO HATUA YA MWISHO WA SWALA YAKO) kama tutakavyoiona
hivi punde.
DHIKRI KTK SALAM
Mwenye kuswali,anatakiwa katika Rakaa ya mwisho ya swala yake,na baada ya kusoma
Tashah-hud,atoe salam na baada ya salam hiyo swala yake itakuwa
imefikia mwisho.Na ambacho ni wajibu ktk salam hiyo-(au tuseme:Sehemu ya
wajibu ktk salam)-anachotakiwa kukisoma bada ya kusoma tashahhud hii
(أشهدُ أن لا إله إلا اللهُ وَحدَهُ لا شَرِيک لهُ وأشهدُ أنَّ محمَّداً عبدُهُ وَرَسُولُهُ اللهُمَّ صلِّ علی محمَّدٍ وَ آل محمَّدٍ.) ni kama ifuatavyo:
“ASSALAM ALAINA WA ALA IBADILLAH SWALIHINA, ASSALAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH”.
(السَّلام علينا وعلی عباد الله الصَّالحين،السَّلام عليکُم ورحمة اللهِ وبرکاته).
Hiyo ndiyo salam ya wajibu ktk swala,lakini ni mustahabu kabla ya salam hizi mbili utangulize salam salam hii ifuatayo:
“ASSALAM ALAIKA AYYUHAN-NABIYYU WARAHMATULLAH WABARAKATUH”:
(السَّلام عليک أيُّها النَّبيُّ ورحمةُ اللهِ وبرکاتهُ).
Hivyo kwa ujumla (ukichukua sehemu ya wajibu ktk salam pamoja na salam hii ambayo ni mustahabu) salam utaianza namna hii kama ifuatavyo:
{ASSALAM
ALAIKA AYYUHAN-NABIYYU WARAHMATULLAH WABARAKATUH,ASSALAM ALAINA WA ALA
IBADILLAH SWALIHINA, ASSALAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH}.
(السَّلام
عليک أيُّها النَّبيُّ ورحمةُ اللهِ وبرکاتهُ). (السَّلام علينا وعلی عباد
الله الصَّالحين،السَّلام عليکُم ورحمة اللهِ وبرکاته).
Na hapo swala yako itakuwa imeisha,na baada ya kumaliza swala yako,ni mustahabu useme: ”ALLAH AKBAR” mara tatu.
Salam
ni sehemu ya swala,na swala haitimii ispokuwa kwa kuelekea Qibla ,kwa
maana kwamba mwenye kuswali anatakiwa kuhakikisha mwili wake na uso wake
vyote vimeelekea Qibla anapokuwa kwenye swala, mwanzo wa swala hadi
mwisho wa swala.
Kwa
mantiki hiyo ikitokea akapinda na kukiacha Qibla,au akageuza uso wake
kutoka Qibla na kuuelekeza sehemu nyingi,kulia au kushoto,basi swala
yake itakuwa batili.Hivyo basi,maadam tayari mwenye kuswali kaisha ingia
kwenye swala kwa kutoa Takbiratul-Ihram,basi anahesabiwa kuwa yuko
tayari ndani ya swali ambapo ni lazima azingatie (muda wote akiwa ktk
swala) kuelekea Qibla mwanzo hadi mwisho wa swala.
Na
tumesema mwisho wa swala ni salam,kwa maana kwamba salam nayo ni sehemu
ya swala,imo ndani ya swala,hivyo hutakiwi kuitoa salam pasina kuelekea
Qibla,kama ambavyo hutakiwi kutoa Takbiratul-ihram (ambayo ndiyo mwanzo
wa swala) kwa kutoelekea Qibla.
Hivyo,ile
kutoa salam kwa kugeuza shingo kulia na kushoto,inahesabika umetoka ktk
Qibla,na kutoka ktk qibla kunabatilisha swala,hivyo salam ktk swala
inatolewa ktk hali ya kuelekeza uso Qibla.Na ieleweke wazi kwamba sio
wajibu wala sio mustahabu kugeuza shingo kulia na kushoto unapokuwa
unatoa salam.
Na
anakosea anayesema kuwa salam si ktk swala,bali salam ni katika swala
kama ilivyo Takbiratul-Ihram,Rukuu,sujuud tahshah-hud,kama ambavyo Rukuu
au Takbiratul-ihram au Sujud ….hutakiwi kuitoa pasina kuelekea Qibla
kadhalika Salam,hutakiwi kuitoa pasina kuelekeza uso wako Qibla.Na
tumesema ni Mustahabu ukimaliza swala yako:Kutoa Takbira kwa kurudia
mara tatu,narudia tena: Ni mustahab (na sio wajib) utoe TAKBIR mara tatu
ukisema: ALLAH AKBA (الله أکبر).
Mwisho
No comments:
Post a Comment