- Taqwa - Tazkiyyah
SWALI:
Mimi
ni msichana wa kiislam nina umri wa miaka 25 naomba mnisaidie nahitaji
kujua dua za kuomba na sala za kusali kwaajili ya kutubu madhambi yangu
kwa Allah.nahitaji kurudi kwa mola wangu
wabillahi Tawfiq
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)
na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tumepokea swali lako na tumefurahi sana kuona kwamba wako ndugu zetu kama wewe wenye kufanya makosa lakini AlhamduliLLaah wanatambua makosa yao na kutaka kurudi kwa Mola wao. Kwa hiyo tambua
kuwa hiyo ni neema kwako kutoka kwa Mola wako kwamba Amekupenda hadi
Akakuonyesha uongofu wa kutambua makosa yako hata utukabili sisi utake
kujua vipi utubu.
Hivyo,
jambo la kwanza linalokupasa ni kumshukuru Allaah (Subhaanahu Wa
Ta'ala) kwa Kukuzindua ukatambua kuwa uko makosani kabla ya adhabu Yake
au mauti kukufika. Vile vile kupata uongofu katika umri kama
huo pia ni jambo la kumshukuru Allaah kwani wengi huendelea na maasi na
kuendelea kuchuma madhambi hadi wanafikia katika umri mkubwa. Yote hayo
ni neema kutoka kwa Mola wako unapasa umshukuru sana kila wakati.
Kuomba Maghfirah unaweza kuswali Rakaa mbili tu kwa nia moyoni ya kuomba Tawbah kwa Mola wako kama utakavyoona dalili katika mada za Tawbah tunazokuwekea viungo vyake chini.
Ama
du’aa, ziko mbali mbali ambazo hata Mitume waliomba walipokuwa
wakifanya makosa au katika kawaida ya kumdhukuru Allaah, pamoja na
adhkaar mbali mbali alizotufunza Mtume (Swallah Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam)
Du’aa
ifuatayo ambayo inaitwa ‘Sayyidul-Istighfaar’ (Bwana wa Kuomba
Maghfirah) inapasa uisome kila mara na katika usimulizi Swahiyh ni
kwamba pindi ukiisoma asubuhi ikawa ni ajali yako kuondoka duniani basi
utaingia Peponi. Na pindi ukiisoma jioni ikawa usiku huo ni siku ya
kuondoka duniani basi utaingia Peponi. Hivyo inampasa kila Muislamu awe
anaidumisha du’aa hii kila siku asubuhi na jioni:
اللّهـمَّ
أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك ،
وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت ، أَعـوذُبِكَ مِنْ
شَـرِّ ما صَنَـعْت ، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ
بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .
‘Allaahumma Anta Rabiiy laa Ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘Abduka wa ana ‘alaa ‘Ahdika wa
Wa’dika mastatwa’tu, A’uudhu Bika min sharri maa Swana’tu, abu-u Laka
Bini’matika ‘alayya wa abu-u bidhanbiy, Faghfir-liy fainnahu laa
yaghfirudh-dhunuuba illa Anta’
Ee
Allaah! Wewe ni Mola wangu, hapana mola Apasaye kuabudiwa kwa haki ila
Wewe, Umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako,
na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda Kwako kutokana na shari
ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa Kunineemesha, na nakiri kwa
madhambi yangu, basi nakuomba Unisamehe kwani hasamehe madhambi ila
Wewe”
Vile vile:
Du’aa ya kusoma baada ya Tashahhud na kabla ya kutoa Salaam katika Swalah:
اللّهُـمَّ
إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ
إِلاّ أَنْت ، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني،
إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم
Allaahuuma
inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman-kathiyran wa laa yaghfirudh-dhunuuba
illa Anta. Faghfir-liy maghfiratam-min ‘Indika War-Hamniy, Innaka
Antal-Ghafuurur-Rahiym.
‘Ee Allaah hakika
mimi nimejidhulumu nafsi yangu, dhulma kubwa, na hasamehe madhambi ila
Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka Kwako, na Unirehemu, hakika Wewe ni
mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu’
Zifuatazo
pia ni du’aa chache kutoka katika Qur-aan ambazo tunazinukuu kwa wepesi
wako, lakini ingia katika kiungo kifutacho utapata zaidi ya hizo:
Duaa Za Qur-aan Maana na Matamshi Yake
Du’aa aliyoomba baba yetu Aadam alipofanya makosa ya kumfuata ibliys.
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ
Rabbana Dhwalamnaa Anfusanaa Wail-Lam Taghfir-Lanaa Watarhamnaa Lanakuunanna Minal-Khaasiriyn.
Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika [Al-A'araaf: 23]
Du’aa Ya Nabii Yuunus (‘Alayhis-Salaam) alipokuwa tumboni mwa nyangumi:
لا إِلَهَ إِلا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ
Laa Ilaaha Illa Anta Subhaanaka Inniy Kuntu Minadh-Dhwaalimiyn
((Hapana mungu isipokuwa Wewe Subhanaka Uliyetakasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu))] [Al-Anbiyaa: 87]
رَبَّنَا
لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ
عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا
رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا
وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى
الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (البقرة 286)
Rabbanaa
Laa Tuaakhidhnaa In Nasiynaa Aw Akhtwa-anaa Rabbana Walaa Tahmil
'Alaynaa Iswran Kamaa Hamaltahu 'Alal-Ladhiyna Min Qablinaa Rabbanaa
Walaa Tuhammilnaa Maa Laa Twaaqata Lanaa-Bih, Wa'fu 'Annaa Waghfir
Lanaa Warhamnaa Anta Mawlaana Fanswurnaa 'Alal-Qawmil Kaafiriyn.
Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama
ulio wabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike
tusiyoyaweza, na Utusamehe, na Utughufirie, na Uturehemu. Wewe Ndiye
Mlinzi wetu. Basi Tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. [Al-Baqarah: 286]
Na
muhimu zaidi ya hayo ni kuwa usome mada zinazohusu Tawbah, vipi kufanya
Tawbah, masharti yake na fadhila zake ambazo zote utazipata katika
kiungo kifuatacho:
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Azidi Kukupa uongofu ubakie katika taqwa na uwe miongoni mwa waja Wake wema. Aamiyn.
Na Allaah Anajua zaidi
No comments:
Post a Comment